Mahakama ya juu nchini Poland imekataa kanuni ya uzito wa sheria za Umoja wa Ulaya juu ya sheria za nchi hiyo katika baadhi ya masuala ya kisheria.
Katika uamuzi huo ambao ni changamoto kubwa kwa Umoja wa Ulaya, mahakama hiyo ya katiba imesema baadhi ya sheria za umoja huo zinakinzana na katiba ya Poland.
Imesema majaji wa Poland hawapaswi kutumia sheria za Umoja wa Ulaya kutilia shaka uhuru wa maamuzi ya wenzao.
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels imesema imeupokea uamuzi huo wa mahakama ya Poland kwa wasiwasi mkubwa.
Shauri la kupinga ukuu wa sheria za Umoja wa Ulaya juu ya sheria za kitaifa liliwasilishwa na Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki, akiwa kiongozi wa kwanza kufanya hivyo katika historia ya umoja huo wenye nchi 27 wanachama.
No comments:
Post a Comment