Search This Blog

Monday, October 18, 2021

Mafuriko yauwa watu 25 India


Watu 25 wamepoteza maisha baada ya kutokea maporomoko ya ardhi na mafuriko ambayo yametokana na mvua kubwa huko kusini/mashariki mwa India. Taarifa za serikali zinasema timu za uokozi zimefanikiwa kuwaokoa watu kwenye matope huku ndege za kijeshi zikiwa zinatoa msaada wa dharura. 
 
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP, miili ya watu 11 ilipatikana katika wilaya ya Idukki na mingine 14 wilaya ya Kottayam. Waziri Mkuu wa jimbo ambalo limeathiriwa zaidi la Kerala, Pinarayi Vijayan alisema maelfu ya watu waliookolewa wamepatiwa hifadhi katika kambi 100 tofauti zilitengwa katika maeneo ya jimbo hilo. 
 
Mamlaka ya hali ya hewa nchini India imetabiri kwamba mvua kubwa katika maeneo hayo itaanza kupungua leo hii. Mwaka 2018 watu 500 walipoteza maisha katika jimbo la Kerala, baada ya jimbo hilo kukumbwa na mafuko mabaya zaidi kutoka katika karne moja.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...