Search This Blog

Saturday, October 2, 2021

Kilo ya misumari, visu na komeo na bisibisi vyaondolewa ndani ya tumbo la mwanaume Lithuania

Madaktari wa upasuaji wamepigwa na butwaa baada ya kupata takriban kilo moja ya misumari , visu, bisibisi na komeo tumboni mwa mgonjwa mmoja aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi akilalamikia kuumwa na tumbo.

Madaktari nchini Lithuania wameondoa kilo ya moja ya misumari, visu nakomeo au skruu kutoka kwa mwanaume, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo. Mwanaume huyo amekuwa akimeza vyuma hivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kuacha kunywa pombem wamesema madaktari. Baadhi ya vifaa hivyo vya chuma viliondolewa wakati wa upasuaji uliofanyika katika hospitali ya Chuo kikuu cha Klaipeda University vilikuwa na urefu wa sentimita 10(inchi 4), kwa mujibu wa mtangazaji wa chombo cha habari cha umma cha Lithuania LRT.Daktari bingwa wa upasuaji Sarunas Dailidenas aliuita upasuaji huo "kisa cha kipekee". Katika makala yake kuhusu kisa hicho iliyochapishwa kwa lughaya Kilithuania, LRT ilichapisha picha aliyopigwa wakati wa upasuaji, huku ikionekana sinia iliyojaa vifaa vya chuma vilivyotolewa tumboni mwake, baada ya saa tatu za upasuaji. Mwanaume huyo alipelekwa kwa gari la kubebea wagonjwa katika hospitali iliyopo kwenye mwambao wa bahari ya Baltic akiwa na maumivu makali ya tumbo. Kwa sasa anaripotiwa kuwa katika hali nzuri, na anaendelea kufuatiliwa katika hospitali hiyo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...