Search This Blog

Sunday, October 10, 2021

Kansela wa Austria kujiuzulu kwa kashfa ya rushwa

 


Kansela wa Austria Sebastian Kurz ametangaza kuwa atajiuzulu nafasi yake kutokana na shinikizo la kuhusishwa na tuhuma za ufisadi. 

Kurz mwenye umri wa miaka 35, aliyengia madarakani 2017 na kuwa kijana mdogo zaidi duniani aliyechaguliwa kidemokrasia amesema anataka kutoa fursa ya kuepusha vurugu.

Shinikizo la mwanasiasa huyo lilitokana na hatua ya mapema wiki hii ya mwendeshamashitaka mkuu wa Austria kusema Kansela Kurz na watu wengine tisa walikuwa wakichunguzwa kwa rushwa baada ya wapelelezi kufanya msako katika ofisi za chama tawala.

Wote hao kwa pamoja wanachunguzwa kwa tuhuma ya kutumia pesa ya serikali katika kipindi cha kati ya miaka ya 2016 na 2018 kushiriki rushwa ya kufanikisha vyombo vya habari kuwaandika vizuri.

Hata hivyo, Kurz amesema tuhuma zote dhidi yake ni za uongo, na kwamba yupo tayari kuzitolea ufafanuzi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...