MBUNGE wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ni miongoni mwa viongozi ambao wamejitokeza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention jijini Dodoma.
"Ni wajibu wetu kuwa hapa na kumuunga mkono Rais wetu kipenzi Samia Suluhu Hassan katika azma yake ya kuliinua Taifa hili kiuchumi na kulilinda dhidi ya UVIKO-19, sisi Wanawake wa Dodoma tunamuelewa na tunasimama nae," Mbunge Ditopile.
No comments:
Post a Comment