Search This Blog

Monday, October 4, 2021

Algeria yapiga marufuku ndege za Ufaransa kuruka kwenye anga yake


Mzozo wa kidiplomasia kati ya Algeria na Ufaransa ulishika kasi jana baada ya Algeria kupiga marufuku ndege za jeshi za Ufaransa katika anga yake. Hatua hiyo ni jibu la hivi karibuni kuhusiano na mzozo wa visa na matamshi makali ya ukosoaji ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. 
 
Wiki iliyopita Algeria ilikasirika baada ya Ufaransa kusema itapunguza idadi ya visa inayowapa raia wa Algeria, Morocco na Tunisia. 
 
Ufaransa imesema imefanya uamuzi huo kutokana na kwamba makoloni yake ya zamani hayachukui hatua za kutosha kuruhusu wahamiaji haramu nchini Ufaransa warudishwe walipotokea. 
 
Ndege za Ufaransa mara kwa mara huruka kwenye anga ya Algeria zikielekea kwenye eneo la Sahel magharibi mwa Afrika, ambapo wanajeshi wake wanasaidia kupambana na makundi ya kijihadi kama sehemu ya operesheni yake ya Barkhane.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...