Algeria imelishutumu koloni lake la zamani Ufaransa kwa mauaji ya halaiki na kutangaza kumrejesha nyumbani Balozi wake mjini Paris, ikikasirishwa na kile ilichosema ni matamshi yasiokubalika kutoka kwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Kulingana na mashirika ya habari ya Ufaransa, Macron hivi karibuni alitoa tamko kuhusu mfumo wa serikali unaoendeshwa kikoloni nchini Algeria.
Taarifa kutoka ofisi ya rais imesema matamshi hayo hayakubaliki, yanaingilia masuala ya ndani ya Algeria na ni dharau kwa wale waliouwawa wakipigania uhuru kutoka kwa Ufaransa.
Mvutano kati ya mataifa hayo mawili uliongezeka pale Ufaransa ilipochukua hatua ya kupunguza visa kwa watu wa Kaskazini mwa Afrika ikiwemo Algeria, kufuatia serikali katika eneo hilo kukataa kuchukua wahamiaji waliofukuzwa Ufaransa.

No comments:
Post a Comment