Search This Blog

Thursday, October 7, 2021

Abu Zubaydah: Jasusi wa zamani wa CIA ataka mshukiwa wa ugaidi aliyemkamata miaka 20 iliyopita kuachiliwa huru

Afisa wa zamani wa CIA aliyegeuka na kuwa mwanaharakati wa kupinga mateso dhidi ya washukiwa wa ugaidi ametaka kuachiliwa kwa mtuhumiwa wa ugaidi aliyemkamata karibu miaka 20 iliyopita.

John Kiriakou aliambia BBC kwamba mateso na kufungwa kwa mshukiwa wa al-Qaeda Abu Zubaydah imekuwa "zaidi ya adhabu ya kutosha".

Wito wa kuachiliwa kwa Bw Zubaydah kutoka chini ya ulinzi wa Marekani ulikuja wakati Mahakama ya juu zaidi iliposikia hoja Jumatano kuhusu uwezo wa serikali ya Marekani kuweka usiri wa ushahidi wa mateso.

Kuzuiliwa kwa Bw Zubaydah ni chanzo cha kesi hiyo mbele ya korti hiyo ya juu zaidi

Kufuatia kukamatwa kwake 2002 huko Pakistan, Mpalestina huyo amedai kwamba alikuwa ameteswa kwa kumwagiwa maji usoni katika mbinu inayojulikana kama waterboarding , alipigwa, alikoseshwa usingizi, alitengwa na kuwekwa katika "nafasi za dhiki" wakati wa kuhojiwa kwenye "vituo vya siri " vya CIA huko Poland kabla ya kuhamishiwa kizuizini huko Guantanamo Bay, ambapo ameshikiliwa bila kushtakiwa tangu 2006.

Vituo hivyo vya siri ni mtandao wa maeneo ulimwenguni kote yaliyotumiwa na CIA kuwahoji washukiwa wa ugaidi katika miaka iliyofuata mashambulio ya 11 Septemba 2001.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...