Search This Blog

Saturday, September 25, 2021

Zaidi ya watu 350,000 wamefariki katika vita ya Syria


Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti yake kwamba zaidi ya watu 350,000 wameuawa katika mzozo wa Syria ambao umedumu kwa muongo mmoja. 
 
Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, amesema takwimu hizo sio idadi kamili ya vifo vilivyotokana na mzozo huko Syria, bali inawakilisha takwimu za chini ambazo zimethibitishwa. 
 
Tathmini ya Umoja wa Mataifa inaashiria kuwa idadi halisi ya watu waliouawa kati ya Machi 2011, wakati vuguvugu la uasi lilipoanza Syria na Machi 2021 ilikuwa kubwa. Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watoto 27,000 wamepoteza maisha katika mzozo huo. 
 
Miezi sita iliyopita shirika linalofuatilia haki za binadamu la Syria, liliorodhesha vifo 388,000. Vikosi tiifu kwa rais wa Syria Bashar al Assad kwa hivi sasa vinadhibiti asilimia 70 ya maeneo ya Syria.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...