Search This Blog

Wednesday, September 29, 2021

Waziri Ummy awataka TARURA kutimizia azma ya Rais Samia kwa vitendo







Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutimiza azma ya Rais Samia kwa kusimamia ujenzi wa barabara kwa ubora kufuatia ongezeko la bajeti kwa mwaka 2021/22.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) mapema leo jijini Dodoma.

Amesema matamanio ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona miundombinu ya barabara inaboreshwa ndio maana ameongeza bajeti kutoka Sh bilioni 277 mpaka Sh bilioni 966 kwa mwaka wa fedha 2021/22.

“ Ongezeko la bajeti ni kubwa inatakiwa kazi itakayofanyika ionekane na iwe na ubora na tuweze kuacha alama na kumbukumbu kwa kazi kubwa aliyoifanya Mhe. Samia Suluhu kupitia Serikali ya Awamu ya Sita,” alisema Mhe. Ummy.

Aliongeza kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hasan wakati akufungua Mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa alisisitiza  kwenye thamani ya fedha za miradi inayotekelezwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na akatuagiza kuhakikisha thamani ya fedha ionekane kwenye miradi yote tunayoitekeleza nasisitiza kwenu ubora wa Barabara zinazoenda kujengwa ukaonekane.

“Katika mpango mkakati wenu mliojiwekea wa Miaka mitano mmeweka kujenga Barabara za Lami zenye urefu wa Km 1455 nikizigawanya kwa mwaka ni kama Km 291 nataka kuziona barabara zikijengwa kwa ubora wa hali ya juu” Mhe Ummy.

Halkadhalika kwenye barabara za udongo mtandao wa barabara uliopo hivi sasa ni km 29,000 lakin mpango wa miaka mitano ni kujenga barabara za changarawe zenye urefu wa kilometa 100,200 niwatake mzingatie ubora wa katika ujenzi wa barabara hizi.

Pia aliwataka TARURa kuweka kipengele cha tafiti katika bajeti zao ili kuweza kupata teknolojia nzuri itakayotusaidia kujenga barabara zenye ubora na zitakazodumu kwa muda mrefu kwa gharama nafuu.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...