Search This Blog

Monday, September 20, 2021

Waziri mkuu wa Uingereza alenga kurekebisha uhusiano na Ufaransa


Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson yupo katika jitihada ya kurekebisha mahusino ya taifa lake na Ufaransa baada ya kufanyika biashara ya pamoja ya nyambizi ya nyuklia kati ya Marekani, Uingereza na Australia.
 
 Pamoja na kwamba hatua hiyo imeigadhibisha Ufaransa, lakini Johnson akiwa njiani kuelekea New York, Marekani amenukuliwa na vyombo vya habari akisema Uingereza inajivunia mahusiano yake ya Ufaransa. 
 
Rekodi zinaonesha Uingereza na Ufaransa zinashirikiana katika operesheni za pamoja nchini Mali na kwenye mataifa ya Baltiki lakini pia katika programu kadhaa za pamoja za majiribio ya kinyuklia.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...