Urusi imeanza hii leo zoezi la siku tatu la upigaji kura katika uchaguzi wa bunge ambao hautazamiwi kubadili chochote katika sura ya siasa za taifa hilo.
Hakuna matarajio kwamba chama cha United Russia, kinachomuunga mkono Rais Vladmir Putin, kitapoteza udhibiti wake wa bunge la taifa linalojulikana kama Duma.
Maswali makuu, hata hivyo, ni iwapo chama hicho kitabakisha wingi wake wa sasa wa theluthi mbili unaokiruhusu kubadili katiba; iwapo uitikiaji mdogo wa wapigakura utafifisha hadhi ya chama hicho; na iwapo mkakati wa Upigaji Kura wa Kijanja wa kiongozi wa upinzani aliefungwa Alexei Navalny, utadhihirisha kuwa sahihi dhidi ya chama hicho.
Rais Putin amewahimiza Warusi kupiga kura, akisema katika ujumbe wa vidio jana Alhamis, kuwa uchaguzi wa muundo mpya wa bunge la Duma ndiyo tukio muhimu zaidi katika maisha ya jamii na taifa lao.
Wapigakura wanatazamiwa kupiga kura zao hadi siku ya Jumapili.

No comments:
Post a Comment