Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wameelezea azma yao ya kuendeleza ushirikiano wa karibu kati ya Ufaransa na Ujerumani kwenye masuala ya kimataifa.
Kwenye mkutano mjini Paris, jana jioni, viongozi hao wawili walijadili masuala kama vile hali nchini Afghanistan na uhusiano wa Ulaya na mataifa jirani ya mashariki.
Angalizo hasa la mazungumzo kati ya wawili hao lilikuwa hali nchini Afghanistan. Kabla ya mazungumzo hayo, Merkel alisema walitaka kujadili nini maana ya kujitoa kwa NATO nchini Afghanistan kwa jumbe za baadae katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Macron aliongeza kuwa walitaka kuzungumzia madhara ambayo Umoja wa Ulaya umejifunza kutokana na hali hiyo.
Merkel anatarajiwa kustafu baadae mwezi huu baada ya miaka 16 madarakani, wakati bunge jipya litakapochaguliwa. Lakini Macron alihakikisha kuwa hii bado siyo ziara yake ya mwisho.

No comments:
Post a Comment