Search This Blog

Tuesday, September 21, 2021

Wanaolimpiki wa Uganda wapandishwa vyeo katika jeshi la polisi

Maafisa wanne wa polisi walioiwakilisha Uganda katika michezo ya Olimpiki wamepandishwa vyeo na na inspekta jenerali.

Mshindi wa nishani ya dhahabu Chemutai Peruth amepandishwa cheo kutoka askari wa kawaida hadi inspekta wa polisi.

Mwanaolimpiki Chelangat Mercyline amepandishwa daraja kutoka cheo cha naimbu inspekata hadi inspekta.

Chemutai Immaculate amepandishwa cheo kutoko koplo hadi sajenti naye Shida Renny akipandishwa cheo kuwa koplo kutoka askari wa kawaida.

Cheo cha mshindi wa dhahabu Cheptegei Joshua na mkufunzi wake Njia Benjaminkutoka inspekta hasi naibu mkuu wa polisi kinafuatiliwa.

Inspecta jenerali amesema wanariadha hao "wanatuzwa kwa mafanikio makubwa na furaha waliyoileta taasisi hiyo na nchi".

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema mwezi Augosti kwamba wanariadha walioshinda medali katika michezo ya Olimpiki mjini Tokyo watapewa magari na nyumba.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...