Search This Blog

Thursday, September 2, 2021

Walimu wakuu matatani baada ya picha ya wanafunzi waliofungwa kwenye mti kuvuja Kenya


Kikosi kazi cha mashirika mengi kimeamuru ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kitaanzisha uchunguzi kuhusu tukio la walimu wawili wakuu wa shule moja huko Laikipia Magharibi nchini Kenya wanaodaiwa kuwafunga wanafunzi watatu kwenye mti kama adhabu. Televisheni ya Citizen nchini Kenya imeripoti.

Kikosi kazi kinachoongozwa na naibu kamishna wa eneo la Nyahururu Moses Muroki alitumia siku ya Jumatano kusikiliza maoni ya walimu na wanafunzi kuhusu tukio hilo lililotolea Ijumaa iliyopita.

Bw. Maina anashutumiwa kuwafunga kwa kamba kwenye mti wanafunzi watatu Ijumaa iliyopita ikiwa ni adhabu kwa kutega shule, kabla ya kuwapiga picha ambazo zilisambaa mitandaoni.

Inadaiwa kuwa baadaye alizituma picha hizo kwenye kundi la WhatsApp la walimu kabla ya mmoja wao kuzivujisha picha hizo kwenye mitandao ya kijamii. Televisheni ya Citizen ilieleza.

Tukio hilo sasa linafanyiwa uchunguzi na mamlaka zimesema hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya walimu hao iwapo watakutwa na hatia.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...