
Mtangazaji wa kipindi cha Televisheni cha Ivory Coast amepewa adhabu ya kifungo cha miezi 12 mahakama ya Abidjan kwa "kushadadia ubakaji".
Pia alitozwa faini ya dola 3,600 za Marekani. Yves de Mbella alitangaza kipindi ambacho mbakaji wa zamani aliyehukumiwa Kader Traoré alionesha kwa kutumia mwanasesere jinsi alivyowadhalilisha wanawake.
De Mbella alicheka na kufanya mzaha huku akimsaidia mtu huyo kumuweka mwanasesere huyo kwenye sakafu na kujifanya kuibaka.
Karibu watu 50,000 walitia saini malalamiko kwa kukemea kitendo hicho.
Siku ya Jumatano mahakama pia ilimhukumu Traoré miezi 24 gerezani na kumtoza faini ya faranga 500,000 kwa makosa hayo hayo.
No comments:
Post a Comment