Wakili wa R Kelly amemlinganisha na kiongozi wa haki za kiraia Martin Luther King Jr katika hoja ya mwisho ya kesi ya dhulma za ngono dhidi ya mwimbaji huyo.
Deveraux Cannick alisema wanaume wote waliwajibisha serikali na aliwahimiza mawakili kuwa na ujasiri.
Mwimbaji, 54, anakanusha mashtaka yote dhidi yake katika kesi hiyo.
Mwendesha mashtaka alimaliza hoja yake kwa ujumbe rahisi: "Mhukumu", baada ya kusema anapaswa kulipia "maumivu aliyoyasababisha kwa kila mwathiriwa wake".
Kelly, ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, anatuhumiwa kwa kuwanyanyasa kingono wanawake na wasichana wa umri mdogo .
Mashtaka hayo ni pamoja na moja la ujambazi na mashtaka manane ya kusafirisha watu kinyume cha sheria katika majimbo kwa lengo la kufanya mapenzi nao.
Katika wiki tano zilizopita, majaji huko Brooklyn, New York, wamesikia kutoka kwa wanaume na wanawake kadhaa ambao walisema nyota huyo iliwanyang'anya udhibiti, akiamua wakati wa kula, kulala na kwenda bafuni, na kuwashinikiza katika tendo la ngono, ambalo mara nyingi angelirekodi kwa video

No comments:
Post a Comment