Search This Blog

Friday, September 24, 2021

Tetesi za soka kimataifa


Tottenham inaweza kuwa tayari kumuachilia kiungo wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, katika makubaliano ya kubadilishana na raia mwenzake mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial (Express)

Liverpool bado inaweza kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Uingereza wa West Ham Jarrod Bowen. Walihusishwa na ofa ya pauni milioni 20 kwenye dirisha la majira ya joto (Liverpool Echo)

Borussia Dortmund inaweza kuwasilisha ombi la kumajili winga wa Juventus na Italia Federico Chiesa, 23, endapo klabu hiyo ya Bundesliga itampoteza mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, msimu ujao wa joto (Calciomercato - in Italian)

Liverpool pia imejiunga na mbio za kusaini Haaland wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke akikiri itakuwa vigumu kusalia na nyota huyo msimu ujao wa joto. (Mundo Deportivo, via Mail)

Kiungo wa kati wa Real Madrid ya Uhispania Marco Asensio, 25, pia ni miongoni mwa wanaolengwa na Liverpool. (Fichajes.Net, via Sun)

Meneja wa Ureno Paulo Fonseca, 48, anasema hatua yake ya kuisimamia Tottenham ilitibuka kwa sababu mkurugenzi wa michezo Fabio Paratici alitaka Spurs icheze mpira wa 'safu ya kujilinda' (Telegraph - subscription required)

Mlinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 28, hatakimbilia uamuzi juu ya maisha yake ya baadaye, lakini anataka nyongeza ya mshahara ikiwa atakaa Stamford Bridge. (90min

Meneja wa Bayern Munich Julian Nagelsmann anasema bado hajazungumza na mkurugenzi wa michezo Hasan Salihamidzic kumhusu Rudiger, ambaye hana mkataba mpya mwaka ujao (Eurosport)

Arsenal inatarajiwa kumpoteza mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette bure wakati mkataba wake utamalizika msimu wa joto, na Atletico Madrid inavutiwa na mchezaji huyo wa miaka 30. (Le10 Sport, via Mirro

Klabu za Uhispania, Ujerumani na Italia zinavutiwa na Lacazette, wakati West Ham na Crystal Palace zinaweza kumpa nafasi ya kubaki kwenye Ligi Kuu. (90min)

Manchester United wamefanya mawasiliano na Barcelona juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa 24 Ousmane Dembele. (El Nacional, via MEN)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...