Search This Blog

Thursday, September 2, 2021

Tetesi za soka za kimataifa


Mlinzi wa Ivory Coast Serge Aurier, 28, atakuwa huru kuhamia Arsenal baada ya kumaliza kandarasi yake huko Tottenham siku ya mwisho ya uhamisho. (Sky Sports)

Mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 22, ana hasira na Sevilla kwa kutomuuza kwa Chelsea. (Spanish Football Podcast, via Express)

Real Madrid iko tayari kumsaka mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, na mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 22 Kylian Mbappe msimu huu. (Marca, via Mail)

Miamba hiyo ya Uhispania pia wanavutiwa kumleta kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28, Bernabeu kutoka Manchester United. (Marca, via Manchester Evening News)

Azma ya Chelsea ya kumsaka Haaland imepata pingamizi baada ya kuambiwa watalazimika kulipa Pauni 825,000 kwa wiki kwa mshahara wake. (Mirror)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alizuia wachezaji watano kuondoka Old Trafford msimu huu. (Mirror)

Everton imemfuatilia mlinzi wa Mwingereza wa Southampton mwenye umri wa miaka 24 Kyle Walker-Peters katika siku za mwisho za usajili. (Telegraph, via Football Transfer Tavern)

Juventus ilikataa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34, kutoka Manchester United muda mfupi baada ya mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 kuondoka klabuni hapo. (Mirror)

Wolves inapanga kufuatilia tena hali ya mkataba wa winga Adama Traore baada ya kukataa mkataba mara mbili kutoka Tottenham kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania. (Birmingham.Live)

Wakala wa Mariano Diaz amesema kuna "kitu cha kushangaza kilichotokea" kumzuia mshambuliaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 kujiunga na Valencia kutoka Real Madrid. (El Partidazo de Cope, via Football Espana)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...