Search This Blog

Thursday, September 2, 2021

Familia ya Kifalme ya Ubelgiji yakumbwa na Kovid-19


Kesi ya maambukizi ya virusi vya corona (Kovid-19) iligunduliwa katika familia ya kifalme ya Ubelgiji.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Ubelgiji, matokeo ya vipimo vya PCR ya Mfalme Philippe na Malkia Mathilde yalionyesha kuwa hawana maambukizi.

Kama tahadhari, Mfalme na Malkia waliahirisha mikutano yao, ambayo ilitakiwa kufanyika wiki hii na Jumatatu ijayo.

Wakati taarifa hiyo haikufafanua ni nani aliyeambukizwa ugonjwa huo, vyombo vya habari vya ndani ya nchi vilitangaza kuwa virusi hivyo vilionekana kwa mtoto wa mmoja wa wanandoa wa kifalme.

Katika nchi yenye idadi ya watu milioni 11, ambapo watu 25,400 wamekufa kutokana na virusi tangu mwanzo wa janga hilo, asilimia 85.3 ya idadi ya watu walipata dozi moja na asilimia 83.3 walipata dozi mbili za chanjo



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...