Manchester United wamemtambua kiungo wa AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie, 24, kama mbadala wa nyota wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 Paul Pogba, ambaye mkataba wake Old Trafford unamalizika mwaka 2022. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mchezaji mwenza wa Pogba katika timu ya taifa Tanguy Ndombele ni kiungo mwingine kwenye rada ya Manchester United aliyehamia tottenham kwa £ 53.8m mnamo 2019. (Calciomercato - in Italian)
Wakati hatma ya Pogba huko United bado haijulikani, Juventus haipangi kumrudisha Mfaransa huyo Turin. Pogba alishinda mataji manne ya Serie A katika misimu mingi huko Juve kabla ya kurudi Old Trafford mnamo 2016. (Tuttomercatoweb - in Italian)
Mlinzi wa Denmark Andreas Christensen yuko tayari kusaini nyongeza ya mkataba huko Chelsea yenye thamani ya Pauni 120,000 kwa wiki baada ya awali kupewa ofa ya mshahara wa chini kuliko pauni 78,000 (Sun)
Juventus na Atletico Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyomwangalia winga wa Arsenal na England Bukayo Saka, 20. . (Calciomercato - in Italian)
Real Madrid inapanga kumsajili beki wa Paris St-Germain Marquinhos, 27, huku Mbrazil huyo akiwa chini ya mkataba katika kilabu hiyo ya Ufaransa hadi 2024. (Fichajes - in Spanish)
Leeds United bado wanavutiwa na winga wa Uholanzi wa Club Bruges Noa Lang, 22. (Football Insider)
Fiorentina wanajaribu kumfunga mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic kwa mkataba mpya baada ya mchezaji huyo wa miaka 28 kuhusishwa na kuhamia Tottenham msimu ujao wa joto(Gazzetta dello Sport via Sport Witness)
Kiungo wa Uingereza Danny Drinkwater anakiri maisha yake ya Chelsea yamekuwa 'katika hali mbaya' baada ya mchezaji huyo wa miaka 28 kuanza kucheza Reading katika uhamisho wa mkopo wake wa nne mbali na Stamford Bridge (talkSPORT)
Inter Milan wana hamu ya kumuachilia fowadi wa Chile Alexis Sanchez, huku Real Betis na Sevilla wakionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 32. (InterLive - in Italian)

No comments:
Post a Comment