Search This Blog

Sunday, September 26, 2021

Sudan: Wanajeshi wa Ethiopia 'walirudishwa nyuma' baada ya kujaribu kuingia al-Fashaga


Sudan inasema imezima jaribio la majeshi ya Ethiopia "kuingia" katika himaya yake.

Mkuu wa majeshi ya Sudan, Jeneral Abdel Fattah al-Burhan, amesema hii inaonesha jinsi majeshi inavyolinda nchi hiyo kufuatia jaribio la mapinduzi lililotibuka wiki iliyopita.

Katika taarifa yake, Sudan ilisema tukio hilo lilifanyikakatika wilaya ya Umm Barakit.

Jeshi la Ethiopia halijajibu ombi la BBC la kutoa maoni.

Lakini kituo cha Habari cha al- Jazeera kinanukuu serikali ya Ethiopia ikisema:"Tunakanusha harakati za vikosi vyetu kwenye mpaka wa Sudan au kuingia kwao katika eneo lolote."

Umm Barakit liko katika eneo la mpakani la al-Fashaga linalozozaniwa, ambako hali ya taharuki imeonezeka.

Kwa miongo kadhaa, raia wa Ethiopia wamekuwa wakifanya shughuli za kilimo katika ardhi hiyo yenye rotuba inayodaiwa na Sudan.

Uhusiano kati ya Sudan na Ethiopia umezorota zaidi tangu Ethiopia ilipoanza kujaza maji katika bwawa iliyojenga katika Mto Nile na vita kuzuka katika eneo lake la Tigray.

Katika miezi ya hivi karibuni, mapigano yameripotiwa mara kadhaa katika eneo la al-Fashaga.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...