Search This Blog

Sunday, September 26, 2021

Mchezaji wa kimataifa wa Sierra Leone aombwa 'kastaafu au apatane na kiti magurudumu'

 


Jeraha la goti limemlazimu mchezaji wa kimataifa wa Sierra Leone Alhassan Kamara kustaafu mapema akiwa na miaka 28 tu,nakuzima ndoto yake ya kushirika katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Januari mwakani huko Cameroon.

Mara ya mwisho mshambuliaji huyo kucheza soka ya ushindani ilikuwa katika klabu ya IFK Varnamo, ambayo alijiunga nayo mwezi March, wakati ilipocheza dhidi ya Brage katika soka ya la daraja la pili huko Uswidi miezi mitano iliyopita.

"Nilichukua uamuzi huo kulingana na ushauri wa mtaalamu wa goti huko Uswidi ambaye aliniambia niachane na kazi yangu kwani inaweza kuathiri zaidi goti langu na hata nikaishia kwenye kiti cha magurudumu," Kamara aliiambia BBC Michezo Afrika.

"Nilipopata jeraha wakati nikicheza Ugiriki mnamo 2018, niliambiwa pia na madaktari kuwa sitaweza kucheza tena. Lakini sikusikiliza na nilirudi Uswidi ili nirudi uwanjani kucheza.

"Ni uamuzi mgumu kwa sababu haikuwa sehemu ya mpango wangu kumaliza kazi yangu wakati huu. Nimefadhaika na kukosa usingizi. Lakini uamuzi huo ni mzuri kwangu."



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...