Search This Blog

Thursday, September 23, 2021

Somalia yaonesha filamu ya kwanza ya umma ndani ya miaka 30

Somalia imeandaa onyesho lake la kwanza la filamu ya umma ndani ya miaka 30 chini ya usalama mkali- ikileta matumaini ya muamko wa kitamaduni katika nchi hiyo yenye misukosuko.

Onyesho hilo lilifanyika Jumatanokatika Ukumbi wa Kitaifa wa Somalia katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, ambayo ilitumiwa kama kambi ya kijeshi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya ukumbi huo wa sinema kutekwa.

Mashabiki wa sinema walifurahia kutazama filamu mbili fupi zilizoelekezwa na mwelekezaji wa filamu wa Somalia Ibrahim CM, tiketi zikiuzwa kwa dola 10 (£7) kila moja.

Ukumbi huo uliyojengwa mwaka 1967, ulionekana kama kiungo muhimu katika uendelezaji wa utamaduni wa Somalia miaka ya 1970 na 80.

Ulifungwa mwaka 1991, mwanzoni mwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na ulitumiwa kama ngome wababe wa kivita waliokuwa wakipigana upande wa pili wa mji.

Ulifunguliwa tena mnamo 2012 baada ya kukarabatiwa na Ujumbe wa Jumuiya ya Afrika huko Somalia (Amisom) - Lakini ukalipuliwa na wanamgambo wa Kiislam wa al-Shabab, ambao walichukulia burudani ya moja kwa moja na filamu kuwa mbaya kimaadili.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...