Search This Blog
Wednesday, September 22, 2021
Serikali kuokoa bilioni 33 Manunuzi dawa, vifaa tiba nje ya nchi
Na WAMJ.- NJOMBE
Serikali inatarajia kuokoa zaidi ya bilioni 33 ambazo ilikuwa ikitumia kununua dawa na vifaa tiba nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Hayo yalielezwa na waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa ukaguzi wa kiwanda cha kutengeneza mipira, dawa za vidonge na maji kilichopo kijiji Idofi mkoani Njombe.
Dkt. Gwajima amesema kiwanda hicho kinakwenda kuzalisha mipira ya mikononi (Gloves) ambayo kwa kipindi hiki imekuwa tatizo kubwa hasa kutokana naCovid 19.
Amesema mipira hiyo imekuwa shida na ghali na wakati mwingine kukosekana kabisa hivyo kiwanda hicho kinakwenda kutatua tatizo hilo la muda mrefu.
Ameongeza mipira itakayozalishwa kwenye kiwanda hicho ni zaidi ya mipira milioni mia moja na nne ambayo inakidhi mahitaji ya Nchi.
"Mhe.Katibu Mkuu, uwezo wetu wa kuzalisha hapa nchini ulikuwa chini ya asilimia 20 lakini tunakwenda kupandisha uwezo wa uzalishaji kupitia kiwanda hiki" amesema Dkt Gwajima.
Dkt. Gwajima ameongeza kuwa serikali itatumia bilioni 8 .1 kupata huduma ya dawa na vifaa tiba kupitia kiwanda hicho tofauti na sasa ambapo inahitajika bilioni 34.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo amesema ameridhishwa na ujenzi wa kiwanda hicho kwani unakwenda kutatua matatizo ya kukosekana kwa dawa na vifaa tiba hapa nchini.
Amesema yanayofanywa na MSD ni Mapinduzi ya kusaidia nchi kuepuka kutopoteza fedha za kigeni zilizokuwa zinatumika kuagiza dawa nje ya nchi.
"Utaratibu huu wa ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini utasaidia kuokoa zaidi ya bilioni 54.4 ambazo zilikuwa zitumike kununua vifaa hivyo nje ya nchi ndani kipindi cha mwaka mmoja" Amesema Chogolo na Kuongeza.
"Uamuzi wa kushusha kuagiza dawa hizi kutoka 50 mpaka 21 bilioni hayo ni Mapinduzi makubwa" alisisitiza Chongolo.
Naye Mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga yeye ameiomba serikali kuharakisha ulipaji wa fidia kwa wananchi wa kijiji cha Idofi ambao maeneo yao waliyatoa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Amesema wananchi hao wamelitoa zaidi ya shilingi milioni mia nane lakini wanadai kiasi cha fedha ambacho ni zaidi ya bilioni mbili.
"Tunaomba serikali yetu inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wananchi hawa ili waweze kulipwa fidia zao" alisema Sanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment