Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha kusikiliza kesi inayowakabili.
Sabaya akiwa amevaa jezi ya timu ya Yanga na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Septemba 24, 2021 wakikabiliwa na mashtaka matano katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27 ya mwaka 2021 kiwemo kosa la utakatishaji fedha Sh 90 milioni.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo,Sylvester Nyegu,Jackson Macha na Nathan Msuya.

No comments:
Post a Comment