Search This Blog

Tuesday, September 28, 2021

Rais Samia atuma salamu za rambirambi kifo cha Naibu Waziri William Ole Nasha



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kufuatia kifo cha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, William Ole Nasha kilichotokea usiku jana Jumatatu Septemba 27, 2021 jijini Dodoma.

Rais ametumia akaunti yake ya Twitter leo Jumanne Septemba 28, 2021 kuandika ujumbe wa pole kwa wabunge, familia na wananchi kufuatia kifo cha Ole Nasha.

“Nasikitika kuwajulisha kuwa aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Mhe. William Tate Ole Nasha amefariki dunia Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Spika Mhe. Job Ndugai, Wabunge, Familia na Wananchi wa Ngorongoro. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...