
Kabla ya Taliban kuchukua uongozi nchini Afghanistan mwezi uliopita, kulikuwa na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wenye ushawishi ambao walikuwa walipinga vikali sera za kundi hilo.
Lakini tangu Agosti 15, Waafghanistan wamekuwa wakifuta picha na ujumbe wao wa zamani mitandaoni - na wengi wameamua kujiondoa kabisa katika mitandao ya kijamii kabisa kwa hofu ya kulengwa na vikosi vya Taliban.
Ijapokuwa Taliban ilitangaza msamaha wa jumla kwa Waafghanistan wote ambao hapo awali walipigana nao au walikuwa sehemu ya serikali iliyopita, baadhi ya wale waliokimbia nchi hiyo waliambia BBC kwamba hawaliamini kundi hili.
Kumekuwa na ripoti kutoka sehemu mbali mbali za nchi kwamba wapiganaji wa Taliban wamewaua raia baada ya kutekwa kwa mji mkuu wa Kabul, licha ya ahadi ya viongozi wao.
Wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Taliban Mohammad Yaqoob alitoa ujumbe wa sauti akikiri kwamba kumekuwa na visa kadhaa vya "mauaji ya kulipiza kisasi" dhidi ya raia yanayofanywa na wapiganaji wa kundi hilo. Hakutoa maelezo zaidi au kutaja matukio maalum.
HTamko hilo lilizua hofu ya athari inayoweza kutokana machapisho ya mitandao ya kijamii, licha ya Facebook kuanzisha huduma za ziada kwa watumiaji nchini Afghanistan - pamoja na kuwaruhusu kufunga profaili zao na kudhibiti ufikiaji wa yaliyomo.
No comments:
Post a Comment