Search This Blog

Wednesday, September 8, 2021

Rais Samia apewa cheo cha Chifu Mkuu wa Machifu wote wa Tanzania, apewa jina


Umoja wa Watemi wa Kisukuma kwa kushirikiana na Umoja wa Machifu Tanzania wamempa jina la ‘Angaya’ Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan lenye maana ya Nyota Angavu.

Akisoma hotuba leo Jumatano Septemba 8, 2021 mbele ya Rais Samia katika tamasha la Utamaduni linalofanyika Viwanja vya Msalaba Mwekundu Kisesa wilayani Magu Mkoa wa Mwanza, Katibu wa Umoja wa Machifu wa Kisukuma, Mtemi Aaroni Mikomangwa amesema jina hilo ni kutambua mchango wa Serikali anayoiongoza kwa kuthamini na kusimamia utu wa wanyonge pamoja na utamaduni wa Mtanzania.

“Unaothamini kazi, ushirikiano, upendo na utu, tunaishukuru Serikali yako kwa kuthamini na kuenzi michango yetu Watanzania wote ikiwepo kuboresha sera za utamaduni kwa kushirikisha asasi za jadi nasi tu pamoja nawe katika kuinua utamaduni wa Taifa letu,”amesema.

Ameiomba Serikali itambue rasmi machifu wa Tanzania kwa kuwapatia usajili rasmi wa umoja wao ili wawe kitu kimoja akidai machifu wengine bado wanalegalega kwakuwa bado hawajatambuliwa rasmi katika kusaidia mila, desturi na kulinda utamaduni.

Amemuomba Rais Samia pia kuwapatia machifu eneo Dodoma kwa ajili ya kuanzisha ofisi, miradi na kujenga makumbusho ya kitaifa.

“Pamoja na maombi yetu ya kutambuliwa, utekelezaji wa shughuli zetu unakabiliwa na changamoto ya kupoteza ya mazingira na udhibiti wa  nyenzo tulizokuwa tukitumia kwa mfano kituo cha kichifu kilichopo maliya na nyumba zilizojengwa na machifu utemini jijini Mwanza,”

Ametaja changamoto nyingine ni kutopata urahisi wa kupata nyara za Serikali wanazozitumia katika shughuli zao akitolea mfano usinga.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...