Search This Blog

Thursday, September 16, 2021

Msiwatumie waalimu kukaimu nafasi za utendaji wa vijiji, mitaa na kata – Waziri Ummy


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ametoa maelekezo  kwa wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutowatumia  waalimu kukaimu  nafasi za  utendaji wa vijiji, mitaa na kata  bali waachwe  wafanye kazi yao ya kufundisha hasa kutokana na upungufu uliopo wa walimu hapa nchini. 

Akiongea na Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani  Waziri Ummy amesema Wakurugenzi wamekuwa wakiwatumia Waalimu kukaimu nafasi ya utendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata suala hili halikubaliki kwa kuwa mwalimu  ameajiriwa  kwa lengo mahususi  la kufundisha  na sio kufanyakazi za utendaji wa kata, vijiji na Mitaa

“Kunachangamoto ya uhaba wa walimu nchini,hivyo tuwaache walimu wafanye kazi ya kufundisha, kwa kuwa jukumu kubwa la waalimu  ni kufundisha, wasikaimishwe kwenye utendaji wa kata, mitaa na vijiji ” amesisitiza Waziri Ummy

Amesema kuwa Serikali inatambua ipo changamoto ya uhaba wa watendaji wa kata, vijiji na mitaa lakini amewataka Wakurugenzi kuanza kuwatumia watumishi wengine wa kada nyingine wakiwemo, maafisa maendeleo ya jamii ili kupunguza changamoto hiyo.

Aidha amezitaka Halmashauri zenye mapato kuajiri watumishi wa kujitolea kwa muda na pia kuhakikisha Mtendaji kukaimu mitaa miwili wakati halmashauri hizo zinajipanga. Aidha Wizara itawasiliana na Ofisi ya Rais Utumishi kuhusu kupata kibali cha kuajiri Watendaji wa Mitaa, Vijiji na Kata ili kupunguza upungufu uliopo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...