Search This Blog

Wednesday, September 8, 2021

Moto wateketeza wafungwa 41 gerezani



Watu wapatao 41 wamekufa baada ya moto kutokea katika gereza katika gereza la Indonesia lililopo pembezoni mwa mji mkuu wa Jakarta.

Moto huo ulitokea majira ya asubuhi sana siku ya Jumatano katika gereza la Tangerang wakati wafungwa wengi wakiwa wamelala.

Kulikuwa na wafungwa 122 katika gereza C ambalo liliathiriwa na moto.

Ila gereza lote lina wafungwa 2,000 idadi iliyozidi kiwango cha gereza hilo ambacho ni watu 600.

Wafungwa hao wengi walikuwa wanashikiliwa kwa makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya.

Watu kadhaa wanadaiwa kujeruiwa wengine wakiwa kitengo cha mahututi.

Hitilafu ya umeme inadaiwa kuwa chanzo cha moto huo, amesema msemaji wa gereza hilo ingawa amesema pia uchunguzi zaidi unafanyika.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...