Meya wa Mji Mkuu wa Ufaransa Anne Hidalgo amezindua azma yake ya kuwania urais wa Ufaransa akisisitizia masuala ya mazingira na kijamii.
Wakati huo huo, kiongozi wa siasa kali za mrengo wa kulia nchini humo Marine Le Pen naye ameelezea nia yake ya kuichukua afisi hiyo kuu zaidi nchini humo wakati ambapo kinyang'anyiro cha kumuondoa madarakani Emmanuel Macron kinapopamba moto.
Hidalgo mwenye umri wa miaka 62 ni mmoja wa wagombea wachache wa mrengo wa kulia na kushoto anayewania kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Ufaransa.
Rais Macron bado hajathibitisha iwapo atagombea muhula wa pili ila matarajio ya hilo kufanyika ni makubwa. Kura za maoni zinaonyesha kwamba yeye na Le Pen watashinda raundi ya kwanza ya kura kisha amshinde Le Pen katika raundi ya pili kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa mwaka 2017.

No comments:
Post a Comment