Search This Blog

Wednesday, September 1, 2021

Merkel amshambulia mgombea wa Ukansela wa chama cha SPD


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amemkosoa mgombea wa ukansela wa chama cha SPD Olaf Scholz kwa utayari wake wa kushirikiana na chama cha Die Linke. 
 
Merkel amemshambulia Scholz, ambaye pia ni waziri wa fedha, baada ya mgombea huyo kusema hapingi uwezekano wa kuunda muungano na chama cha siasa kali za mrengo wa kushoto Die Linke, baada ya uchaguzi. 
 
Chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union CDU cha Angela Merkel, kimepinga wazo la muungano na chama cha Die Linke kutokana na kile inachokitaja kuwa chama hicho cha siasa kali kina sera ya kigeni isiyokubalika.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...