Search This Blog

Friday, September 24, 2021

Mbunge wa Uganda akamatwa muda mfupi baada ya kutolewa gerezani



Mbunge wa upinzani nchini Ugandan Allan Ssewanyana alikamatwa tena mara baada yakuachiliwa kwa dhamana kutoka jela Alhamisi jioni.

Wakili wake, Mbunge Shamim Malende, anasema hana maelezo yoyote kuhusu aliko mteja wake na anazuiliwa na nani.

Katika kanda ya video iliyoshirikishwa kwenye mitandao ya kijmii, mbunge huyo anaonekana akipita katikati ya kituo cha ukaguzi cha gereza wakati anatoka.

Sekunde chache baada ya kupita kizuizi hicho, gari nyeupe ambalo limepewa jina la ‘drone’, linapita karibu na kusimama ghafla mbele yake... ambapo wanaume sita waliokuwa naa mavazi nyeusi walimshika na kumrusha ndani.

‘Drones’ zilikuwa maarufu msimu wa uchaguzi wa Januari January 2021, kwa kutumiwa kuwashika na kuwaondoa maelfu ya wafuasi wa upinzani, baadhi yao mpaka sasa hawajawahi kuonekana tena.

Mhe. Ssewanyana na mwenzake Muhammad Ssegirinya walipewa dhamana na mahakama mjini Masaka Jumatatu lakini ilichukuwa siku kadhaa kukamilisha utaratibu wa kutolewa kwao gerzani.

Bw. Ssegirinya anasalia gerezani,kwa sababu mmoja wa wadhamini wake hakuwepo kutia saini nyaraka za mahakama.

Wabunge hao wawili wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi, mauaji, na jaribio la mauaji, kuhusiana na wimbi la mauaji ya mapanga katika eneo la Masaka, kati kati mwa Uganda.

Watu wasiopungua 28 waliuawa kati ya Julai na Agosti.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...