Search This Blog

Thursday, September 23, 2021

Marekani yaridhia nyongeza ya chanjo ya Pfizer kwa wazee


Marekani imeridhia nyongeza ya chanjo ya Covid-19 aina ya Pfizer kwa watu wenye zaidi ya umri wa miaka 65, au watu wanaoishi na magonjwa mengine nyemelezi pamoja na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.
 
Tangazo hilo kwa sasa linamaanisha mamilioni ya Wamarekani watakidhi vigezo vya dozi ya tatu, baada ya miezi sita kupita baada ya kukamilisha chanjo yao ya pili.
 
Kwa wale waliotumia chanjo nyingine kama Moderna na Johnson & Johnson watapaswa kusubiri.
 
Uamuzi huo wa nyongeza ya chanjo ya Pfizer umetolewa baada ya juma lililopita jopo huru la wataalamu lililoitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) kuuidhinisha kwa kuupigia kura.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...