Search This Blog

Tuesday, September 7, 2021

Mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa Uyui imewafukuza kazi watumishi


BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui limewafukuza kazi watumishi 15 kwa makosa mbalimbali.

Kauli hiyo imetolelewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba ya Madiwani wenzake na wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani.

Alisema watumishi  hao wamefukuzwa kwa sababu ya  na makosa ya utoro kazini na wengine walikutwa na vyeti vya bandia(vyeti feki).

Ntahondi alisema watuhumiwa 28 waliokuwa waliokuwa wanakakabiriwa na tuhuma mbalimbali wamefutiwa makosa yao baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kuwaingiza hatiani.

Alisema Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Halmashauri hiyo imemwondoa Mtendaji wa Kata ya Nsololo na kuwamgiza Mkurugenzi Mteandaji kupeleka Mtendaji mwingine baada ya kubaini aliyekuwepo kushindwa kumudu majukumu yake.

Ntahondi aliongeza wamemsimisha Fundi Sanifu wa Halmashauri hiyo kupitisha uchunguzi baada ya kubainika mapungufu katika ujenzi wa baadhi ya Maabara  wilayani humo.

Aidha Mwenyekiti huyo aliwaagiza Wakuu wa Idara wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia vema watumishi wanaowasimamia ile waendelee kutoa huduma bora kwa wananchi.

 




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...