Maafisa wa watatu wa zamani wa ujasusi nchini Marekani wamekiri kuipa nchi ya Falme za Kiarabu teknolojia ya udukuzi.
Maafisa hao wamekubali pia kulipa karibu dola milioni 1.7 kutatua mashtaka ya uhalifu dhidi yao katika makubaliano ambayo wizara ya haki Marekani imeyaelezea kama ya kwanza ya aina yake.
Maafisa hao Marc Baier, Ryan Adams na Daniel Gericke wanatuhumiwa kufanya kazi kama mameneja wakuu katika kampuni moja iliyo na makao yake Falme za Kiarabu, iliyokuwa inafanya shughuli za udukuzi kwa niaba ya serikali.
Waendesha mashtaka wanasema, watu hao walipeana teknolojia ya udukuzi na mifumo ya kijasusi ya kukusanya taarifa ambayo ilitumika kudukua kompyuta Marekani na nchi zengine duniani.

No comments:
Post a Comment