Search This Blog

Wednesday, September 15, 2021

Wapiganaji wa Libya wapambana na waasi wa Chad mpakani


Vikosi vitiifu kwa mbabe wa kivita mashariki mwa Libya Khalifa Haftar vimefanya operesheni dhidi ya wanamgambo wa Chad waliojihami katika eneo la mpakani kusini mwa nchi hiyo. 
 
Kulingana na vyombo vya habari vilivyo karibu na Haftar, kikosi maalum cha Tarek ben Ziyad, mojawapo ya kikosi kitiifu kwa Haftar, kimefanya operesheni kubwa dhidi ya mamluki na wanamgambo wa upinzani wa Chad waliokuwa katika eneo la Libya. 
 
Inaripotiwa kwamba mwanajeshi mmoja wa kikosi hicho cha Haftar, ameuwawa na magari kadhaa ya kijeshi kuharibiwa. Makundi kadhaa ya waasi ya Chad yako nchini Libya, Sudan na maeneo ya mipaka ya nchi hizo mbili.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...