Na Maridhia Ngemela, Mwanza.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Ilemela kata ya Kirumba Mkoani Mwanza wamechoshwa na michango ya mitihani na masomo ya ziada kutoka kwa baadhi ya walimu wasiokuwa waaminifu kulazimisha kupatiwa fedha kutoka kwa wazazi.
Hayo yamebainika katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mh.Hassan Masala alipokuwa kwenye kikao cha hadhara kilichofanyika katika kata ya Kirumba mara baada ya kuwapa nafasi wananchi kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali ili aweze kuzitatua na kuzipatia ufumbuzi.
Miongoni mwa wananchi wakipata nafasi ya kuzungumza ni Zubeda Kamala "alisema kuwa, wanafunzi wanachangishwa hela ya mitihani shilingi mia tatu wasipotoa watoto wanachapwa hii imekuwa kero kwa wazazi muda mwingine unakuta hatuna hela na mtoto anaogopa kwenda shule kwasababu hajaelewa hela na wakati Serikali ishatwambia elimu bure"alisema Zubeda.
Naye Mkuu wa Wilaya Hassan Masala amekemea vikali kitendo hicho cha michango ambayo imekuwa kero kwa wazazi kutoendelea kwani Serikali Mila mwezi inatoa fedha kwaajili ya wanafunzi ili waweze kupatiwa elimu bure na siyo kuchangisha michango kutoka kwa wazazi.
Masala alisema, wazazi ni lazima tujue kuwa elimu ni gharama na hatuwezi kukwepa gharama ya kugharamia watoto wetu lakini nilazima tuwaelimishe wananchi waweze kuelewa vitu hivi vya fedha zinazotolewa na Serikali waelezwe mchanganuo wa fedha hizo ambazo zinawasomesha watoto ninashida maafisa elimu wangu hamyasemi haya "alisema Masala.
"Alisema utaratibu wa watoto kuchangishana hatutoukubali nisije kusikia mtoto kafukuzwa shule kwasababu hajachangia hela ya mtihani na masomo ya ziada unataka hela ya masomo ya ziada wakati mwisho wa mwezi mnalipwa mshahara naomba msinijaribu mahubili nikiondoka ndio muendeleze na utaratibu wenu wa kufukuza watoto shule.
Na miongoni mwa kero ambazo wamemueleza Mkuu wa Wilaya ni ukosefu wa maji,umeme na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa sugu na kutopatiwa ufumbuzi.


No comments:
Post a Comment