Search This Blog

Saturday, September 25, 2021

Kiongozi wa kijeshi wa Chad atangaza bunge la mpito


Kiongozi wa kijeshi wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno, ametangaza wajumbe 93 watakaounda Baraza la kitaifa la bunge la mpito. Hatua hiyo inakuja miezi mitano baada ya Mahamat kujitangaza kiongozi kufuatia kifo cha baba yake Idriss Deby Itno. 
 
Baraza hilo limeundwa zaidi na vyama ambavyo awali vilikuwa na uwakilishi katika bunge lililovunjwa, vyama vingine ambavyo havikuwa na uwakilishi na wanachama wa ulinzi na majeshi, mashirika ya kiraia, vijana na wanawake. 
 
Hata hivyo wanachama wa jukwaa la upinzani la Wakit Tamma, au mashirika ya kiraia ambayo yalilaani mapinduzi hayakujumishwa kwenye baraza hilo. Chad imekabiliwa na mapinduzi tangu ilipojipatia uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1960. 
 
Taifa hilo ni mshirika muhimu wa Ufaransa haswa katika mapambano dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali katika eneo la Sahel.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...