Mamlaka ya kijeshi ya Guinea, junta imeamuru benki kufungia akaunti zote zinazohusiana na serikali ili "kupata mali za serikali".
Junta, ambayo ilichukua udhibiti wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, inasema agizo hilo linaathiri akaunti za taasisi na watu binafsi wa serikali inayomaliza muda wake.
Maofisa wa juu wa serikali ya Rais aliyeondolewa madarakani Alpha Condé hawataweza kutumia akaunti zao.
Viongozi wa mapinduzi walichukua madaraka Jumapili, na walisema wanataka kumaliza ufisadi uliokithiri, ukiukwaji wa haki za binadamu na usimamizi mbaya.
Guinean authorities.Jumuiya ya eneo la Magharibi mwa Afrika Ecowas - ambayo inataka katiba kufatwa - imetuma ujumbe wa kutaka kufanya mazungumzo na mamlaka ya Guinea.
Jumuiya hiyo imetaka Rais Condé ambaye ameshikiliwa na jeshi kuachiwa huru.

No comments:
Post a Comment