Idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga Cha Ida nchini Marekani imeongezeka na kufikia 63.
Kimbunga hicho kilitokea mnamo mwezi Agosti 29 kaskazini Mashariki mwa Marekani.
Kimbunga hicho kinachoenda kwa Kasi ya kilomita 241 kwa saa kimeathiri majimbo ya Loissan,New York na Pennsylvania.
Aidha,imeripotiwa kuwa zaidi ya makazi ya watu zaidi ya milioni moja yameachwa bila nguvu za umeme.
Rais wa Marekani Joe Biden amewaahidi waathiriwa msaada kufuatia hasara za kimbunga hicho.

No comments:
Post a Comment