Search This Blog

Saturday, September 25, 2021

Dkt.Gwajima amekagua ujenzi wa jengo maalum la mionzi ya saratani katika hospital ya Rufaa Kanda ya kasikazini KCMC



Waziri Wa Afya Maendekeo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Dorothy Gwajima amekagua ujenzi wa jengo maalum la mionzi ya saratani katika hospital ya Rufaa Kanda ya kasikazini  KCMC  kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi

Dkt Gwajima amesema kuwa serikali imejipanga kuboresha huduma katika hospitaki za kanda ya kasikazini Kilimanjaro,Mbeya Musoma Mwanza Na Hospirali ya Chato ili kuwapunguzia adha wagonjwa kusafiri kwenda jijini Dar es salaam kufuata huduma ya mionzi.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mikakati ya kuboresha huduma za afya mijini na vijijini ikiwemo kujenga majengo maalumu ya mionzi ya saratani ili wagonjwa wapatiwe matibabu kwenye maeneo yao


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...