Search This Blog

Sunday, September 19, 2021

Chama cha Putin kujizolea viti vingi vya bunge

 


Chama cha Rais Vladimir Putin wa Urusi kinatarajiwa kupata ushindi leo na kuendelea kuwa na wingi wa viti bungeni katika siku ya mwisho ya uchaguzi wa bunge ambao wakosoaji wengi wa Ikulu ya Kremlin wamezuiwa kushiriki. 


Chama hicho cha United Russia kinatazamiwa kujizolea idadi kubwa ya viti bungeni, licha ya kuporomoka kwa uungaji mkono wa umma kutokana na hali ngumu ya maisha iliyochangiwa na kuanguka kwa uchumi wa Urusi. 


United Russia inategemea kwa sehemu kubwa umashuhuri wa Rais Putin ambao bado ni mkubwa miongoni mwa wapigakura, licha ya tuhuma zinazouandama utawala wake, ikiwemo ukandamizaji mkubwa dhidi ya upinzani. Kuelekea uchaguzi huo ulioanza siku ya Ijumaa, viongozi wengi wa upinzani na wafuasi wao walikamatwa na vyombo vya dola na kuna ripoti pia za vitendo vya udanganyifu, hususan upigaji wa kura bandia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...