Search This Blog

Thursday, September 16, 2021

Bilioni 53.6 kukamilisha ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 nchini


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema jumla ya shilingi bilioni 53.6 zitatolewa na Serikali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 zilizojengwa nchini.

Ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akikagua  ujenzi wa Hospiatali ya Wilaya ya Kibiti katika ziara ya kikazi aliyoifanya katika, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo

Waziri Ummy amesema kuwa katika kuhakikisha Hospitali za Wilaya zilizojengwa katika awamu ya kwanza zinakamilika serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 800 kwa kila Hospitali ya Wilaya lengo likiwa ni kukamilisha miundombinu ya majengo katika hospitali hizo

Ameendelea kufafanua kuwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi serikali ilipeleka fedha kiasi cha shilingi bilioni 1. 5 kwa ajili ya ujenzi wa majengo saba ya awali, kisha shilingi milioni 300 na sasa shilingi milioni 800 kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu hiyo ili wananchi waweze kupata huduma bora za afya katika maeneo yao.

Aidha, amesema kuwa Serikali imejipanga katika  kuhakikisha vifaa na vifaa tiba vinapatikana kwa wakati ili wananchi waweze kuzitumia Hospitali zetu kikamilifu kwa kuhakikishiwa kuwa huduma bora zinapatikana katika Hospitali za Serikali

Kuhusu uhaba wa watumishi Waziri Ummy amewaagiza Makatibu Tawala wa Mkoa wote nchini kuhakikisha wanafanya msawazo kwa watumishi wote wakiwemo wa sekta ya afya ili kupunguza uhaba wa watumishi katika maeneo yao




 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...