Search This Blog

Monday, August 9, 2021

Wazawa watakiwa kujitokeza kuchangia elimu makwao.


Na Timothy Itembe Mara.


MKUU wa shule ya sekondaro Tarime mkoani Mara,Machota Kora amewataka wazawa kupenda kuchangia shuguli za maendeleo ya elimu Nyumbani kwao na kuwa pindi watoto watakapo elimika wataepuka na kuacha mila kandamizi zilizopitwa na wakati.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake alisema baadhi ya wazawa wameb
arikiwa lakini hawanatabia ya kupenda kuchangia shuguli za maendeleo ya elimu Nyumbani kwao badala yake misaada hiyo wanelekeza katika mikoa mingine huku wakiacha kwao kunaharibika.
 
Mkuu huyo alitumia nafasi hiyo kupongeza kampuni ya nyambari nyangwine publishers iliyopo Jijini Daresalam kwa kuchangia na kutoa msada wa vitabu vya Sayansi vya  ziada na kiada vitakavyochangia kuinua na kuongeza ufaulu wa kitaaluma kwa wanafunzi.
 
Machota alisema kuwa alipokea vitabu hivyo mwezi Mei mwaka huu vyenye dhamani ya shilingi milioni 5.2 kwa ajili ya masomo ya kidato cha Tano na sita ambavyo vitasaidia kitaaluma kuongeza ari ya kuinua taaluma ya elimu kwa wanafunzi.
 
"Tumepokea mwezi mei mwaka huu vitabu vya sayansi na Biashara zaidi ya 196 vya Kiada na ziada kutoka kwa kampuni ya nyambari nyangwine publishers ambaye ni  msamaria mwema na vitasaidia kuwainua na kuwajenga kitaaluma Wanafunzi"alisema Kora.

Mwalimu huyo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wale wote ambao wamefika shuleni hapo wakichangia mali na vitu mbalimbali kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele na shule inainua taaluma ya ufaulu kwa wanafunzi.
 
Kora aliwataja watu wengine walifika shuleni hapo kuchangia kuwa ni pamoja na Tasisi ya kifedha CRDB Banki ambapo walichangia Maji ya kunywa kwa wanafunzi na walimu baada ya shule hiyo kufanya vizuri katika mtihani wa kitaifa mwaka huu wa kidato cha Sita.
 
Nitumie pia nafasi hii kuwashukur
u wafadhili kama vile Mbunge wa jimbo la Tarimne mjini,Michael Kembaki kwa ambapo alitoa shilingi milioni 3 kwa ajili ya walimu kutumia kwenda kutaalii utalii wa ndani katika Visiwa vya Zanzibar ambapo jitihada zinafanyika ili walimu hao waondoke na kwenda kujifunza kama ilivyokusudiwa.
 
Mwalimu huyo aliongeza kuwa shule yake inakabiliwa na nchangamoto ya miundombinu ya Umeme ambapo kwa ujumla wanatumia Jenereta ambayo haimudu matumizi ya shule kwa mda mwafaka kwa hali hiyo anaomba wafadhili watakaoguswa kujitokeza na kuja kutoa msaada na wanafunzi wakasoma kwa raha.
 
Changamoto nyingine ni changamoto ya maji pamoja na kuwa kuna  mfumo wa maji hapo shuleni upo lakini maji hayo yanatoka kidogo kidogo sana na hayakidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo zaidi ya 900 na badala yake wanatumia maji ya kisima cha kupampu.
 
Kora alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali awamu ya sita chini ya Rais wake Samia Suluhu Hasaan katika utekelezaji wa shuguli za maendeleo ambapo shule yake kwa ushirikiano wa viongozi wa ngazi mbalimbali mkoa na wilaya wamefanikiwa kuwa wa 77 kitaifa kati ya shule 610 kwa mwaka 2021 ambapo ufaulu wa Divisheni One walikuwa na 163,11 zilikuwa 135,111,zilikuwa 21,iv zilkuwa00 na 0 zilikuwa 00 matokeo ya mtihani wa kidato cha Sita.
 
Naye Makamu mkuu wa shule ya sekondari Tarime,Werenfrid Shangwe alisema shule yake imefanya vizuri mfulilizo mitihani kwa miaka mitatu bila kushuka ufaulu na kwa mwaka huu imekuwa ya Nne (4) ndani ya shule kumi Bora kimkoa.
 
Mwalimu huyo alitaja matokeo kidato cha Sita Tarime Sekondari kuanzia mwaka 2019 hadi 2021 kuwa mwaka 2019 shule hiyo ilipata divisheni One 30 na kuwa nafasi ya 542 kati ya 594 kitaifa mwaka 2020  Divisheni One 33 na kushika nafasi ya 274 kati ya 586 Kitaifa mwaka 2021 wamepata 163 Divisheni One na kuwa nafasi ya 77 kati ya 610 Kitaifa.
 
Shangwe amemaliza kwa kusema shule yake inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya umeme na maji na kuwa wanakaribisha wahisani watakao guswa kufika na kuchangia Elimu lengo likiwa ni kuongeza ufaulu wa kitaaluma ili kuwa wa kumi Bora kitaifa mwaka 2022.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...