Search This Blog

Monday, August 9, 2021

Naibu Waziri auvaa mgogoro wa Nyandoto


Na Timothy Itembe Mara.
 
Naibu waziri Ardhi Nyumba na mandeleo ya makazi,Angeline Mabula juzi ametatua kero ya mgogoro wa wakazi wa Nyandoto halmashauri ya mji wa Tarime.
 
Mabula alisema kuwa nimesikiliza pande zote mbili na kugundua kuwa halmasauri iliingia kupima maeneo ya watu hao bila kuwashirikisha jambo ambalo lilizua mgogoro.
 
"Mimi nimesikiliza pande zote mbili ambapo nimegundua kuwa halmashauri ilingia kupima maeneo hayo bila kuwashirikisha waliokuwa wamiliki kwa hali hiyo nimesema maeneo niyao na wapimiwe kwa taratibu huku wakiwashirikisha na walipie kwa mda utakao kuwa umepangwa vinginevyo atakayeshindwa kulipia hatua zaidi zitachukuliwa"alisema Mabula.

Mabula alimaliza kwa kusema maeneo yanayolalamikiwa yatakuwa chini ya wamiliki na halmashauri itaende kupima viwanja kupitia wataalamu wa serikali huku wakiwashirikisha wenyeji ambao niwamiliki na viwanja vitakavyopatikana vyote watalipia gharama za upimaji na watapewa mda wa kulipia mda ukipita kwa atakayekuwa ameshindwa kulipia hatua zaidi zitachukuliwa.
 
Wamiliki hao wakiongozwa na viongozi wao walifika mjini Musoma wakilalamika kwa Naibi waziri Ardhi Nyumba na maendele ya makazi baada ya kuikia kuwa atakuwepo mjini hapo kwa shuguli za kiserikali.
 
Mmoja wa walalamikiaji hao Neema Timothy Itembe alisema maeneo yao wanayamiliki kihalali na kuwa halmashauri ya mji wa Tarime inatumia nguvu kuwanyang'anya na kupima viwanja bila kuwashirikisha.
 
Neema aliongeza kusema watu ambao wanamiliki viwanja Nyandoto wanaomba kupimiwa viwanja vyao kama vilivyo na kuvulipia na kuendeleza kwa maendeleo mbalimbali ikiwemo kulima mboga mboga na matunda ili kupata fedha za kuwasomeshea watoto na mahitaji mengine ya kifamilia.
 
Neema aliongeza kusema awali mgogoro huo umekuwa wa mda mrefu na wamefika hadi Ofisi ya mkuu wa mkoa Mara bila mafanikio jambo ambalo majibu yake yamekuwa yakitolewa niyakigugumizi.
Kwa upande wa kulipa kodi ya Ardhi Neema alisema hawana wasiwasi wakipimiwa viwanja hata viwe vingapi watalipia ili kuchangia patp la serilaki.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...