
Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewakamata watu wapato 100 wakiwashukia kuwa watumiaji na wauzaji wa dawa mpya za kulevya.
Rais Felix Tshisekedi ametaka uchunguzi ufanyike kuhusu dawa hizo za kulevya ambazo zinatengeneza katika bomba la kutoa moshi wa gari.
Dawa hizo mpya zinazoitwa 'bombe' ni mchanganyiko unga wa dawa mbalimbali.
Baadhi ya wanaoshukiwa kuwa watumiaji walikamatwa Alhamisi , wakala wa habari wa AFP wameripoti, kuwa walikuwa hawana hatia ila tu walikuwa katika eneo baya na muda usio rafiki.
Mkuu wa Polisi katika uhalifu Alphonse Landu amesema wanawafuatilia wauzaji wa dawa hizo za kulevya za kienyeji mjini Kinshasa, tovuti ya Actualite Congo umeripoti.
Matumizi ya dawa la kulevya DRC ni changamoto kubwa kwa vijana , wizara ya afya ina wasiwasi juu ya dawa hizo mpya za kulevya.
No comments:
Post a Comment