Mkuu wa Wilaya ya Muleba, bw Toba Nguvila amewapongeza vijana wa Chama cha Mapinduzi waliojitolea kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni mkakati wa kuimarisha benki za matofari kwa kila kata, wilayani Muleba.
Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa vijana wa CCM Muleba wa ufyatuaji wa matofali ambayo yatasaidia kupunguza kero za ukosefu wa vyumba vya madarasa na zahanati wilayani humo.
"Nawapongeza sana kwa utayari wenu wa kujitoa kuja kushiriki katika zoezi hili ambalo tutalitekeleza katika kata zote 43 za wilaya ya Muleba. Kwa kujitoa kwenu nami nitahakikisha kuwapa kipaumbele kwa fursa zitakazokuja wilayani kwetu ikiwemo utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta kama sehemu ya motisha" ameeleza Mkuu wa Wilaya.
Kambi hiyo inaundwa na vijana wa Chama cha Mapinduzi wapatao 70 wanaume 55 na wanaweka 15 kutoka katika kata za Ngenge, Ibuga, Muleba Bureza na Kibanga.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Comred Mtwaafu Kantangayo ameeleza kuwa kwa siku mbili wameweza kufyatua jumla ya tofari 12,668.
Uzinduzi huu umefanyika katika kijiji cha Kibanga, kata ya Kibanga leo tarehe 10.08.2021.

No comments:
Post a Comment