Search This Blog

Sunday, August 22, 2021

Uturuki haitaweza kustahamili wimbi la wakimbizi wa Afghanistan - Rais Erdogan

 


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema nchi yake haitaweza kustahamili ongezeko lingine la wahamiaji wanaowasili kutoka Afghanistan. 

Akizungumza kwa njia ya simu na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Erdogan amesema wimbi jipya la wahamiaji halikwepeki iwepo hakuna hatua madhubuti zitakazochukuliwa nchini Afghanistan na Iran. 

Erdogan amemweleza kansela Merkel kuwa Uturuki ambayo tayari inawahifadhi wakimbizi milioni 5 haitaweza kupokea ziada ya wahamiaji. 

Kwenye mazungumzo hayo bibi Merkel amesema kipaumble cha serikali yake kwa sasa ni kuwahamisha watu kutoka Afghanistan. 

Erdogan anaulaumu Umoja wa Ulaya kwa kukwepa pendekezo la Uturuki la kuufanyia marekebisho mkataba baina yao wa mwaka 2016 ulionuwia kudhibiti wingi la wahamiaji kwenye mataifa ya Ulaya kwa kuipatia fedha nchini yake ili kuwapatia hifadhi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...